Waziri Kombo akutana na Makamu wa Rais wa JICA

YOKOHAMA-Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amefanya mazungumzo na Bw. Ando Naoki, Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) pembezoni mwa Mkutano wa Tisa wa TICAD uliofanyika jijini Yokohama.
Mheshimiwa Waziri Kombo amepongeza ushirikiano wa Tanzania na Japan kupitia JICA katika ufadhili wa uendelezaji wa sekta za kilimo,nishati,usafirishaji,afya,maji na uendelezaji wa rasilimali watu.
Katika kikao hicho walikubaliana kuendeleza ushirikiano huo hususani katika sekta za miundombinu bora, uendelezaji wa rasilimali watu, uchumi wa buluu na kilimo hususan teknolojia ya kuongeza thamani malighafi za mazao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news