ARUSHA-Wenyeviti wa Bodi na Wakurugenzi wa Taasisi za Umma wameendelea kumiminika kwenye banda la Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) huku wakivutiwa na miradi mbalimbali ikiwemo ya 711 na Samia Housing Scheme.
Ni katika Kongamano la Wenyeviti wa Bodi na Wakurugenzi wa Taasisi za Umma linaloendelea katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (AICC) jijini Arusha ambalo limefunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Philip Mpango kwa niaba ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Katika banda hilo, viongozi hao wameridhishwa na maelezo ya kina waliyopewa kuhusu miradi hii na kufurahia uwepo wa NHC, kwani banda limekuwa chanzo cha taarifa muhimu na za wazi kuhusu maendeleo ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu nchini.












