GEITA-Wanafunzi kutoka shule mbalimbali mkoani Geita wametembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika Maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Ziara hiyo ililenga kuwapa fursa ya kupata elimu ya kifedha, utambuzi wa alama za usalama katika noti, utunzaji sahihi wa noti hizo pamoja na nafasi ya Benki Kuu katika kusimamia uchumi wa nchi.



