RAIS wa Marekani, Donald Trump ametangaza ushuru mpya kwa bidhaa mbalimbali zinazoagizwa kutoka nje, ikiwemo dawa na malori makubwa ya mizigo.
Ushuru huo unatarajiwa kupanda hadi asilimia 100 kwa baadhi ya dawa, huku malori makubwa yakitozwa ushuru wa asilimia 25 na vifaa vya jikoni na bafuni vikiongezwa ushuru wa asilimia 50.
Hatua hiyo inalenga kulinda masoko ya ndani na kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vya Marekani. Kupitia ukurasa wake wa Truth Social,
Rais Trump alisema bidhaa nyingi kutoka nje zimekuwa zikiuzwa kwa bei nafuu kiasi cha kushusha thamani ya bidhaa za ndani. Hata hivyo, wafanyabiashara nchini humo wamepinga uamuzi huo na kuitaka Ikulu kusitisha ongezeko la ushuru
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo























