BoT:Hati fungani ya Serikali ya miaka 20 mnada Na.01 (20-year treasury bond auction No.01)

Benki Kuu ya Tanzania kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huuza Dhamana za Serikali za muda mrefu (Hati fungani) ikiwa ni njia ya kukopa fedha kutoka kwa ama taasisi au mwananchi mmoja mmoja.

Dhamana za muda mrefu ni zile ambazo muda wake wa kuiva unazidi mwaka mmoja. Dhamana hizi huuzwa kwenye soko la awali kwa njia ya ushindani kupitia minada na baada ya hapo uuzaji wa dhamana hizo hufanywa kwenye soko la upili.

Mwekezaji atanunua Hati fungani kupitia kwa Mawakala ambao ni benki zote za biashara zilizosajiliwa na kupatiwa leseni ya biashara na benki kutoka Benki Kuu ya Tanzania au Mawakala wa soko la Hisa la Dar-es- Salaam waliopatiwa leseni na kusimamiwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana.

Mwekezaji mwenye kiwango cha kuanzia shillingi milioni moja (TZS 1,000,000.00) na kuendelea anaruhusiwa kushiriki katika mnada wa Dhamana za Muda Mrefu (Hati Fungani).

Kabla ya kuwekeza, kila mwekezaji anatakiwa kufungua akaunti maalum ya uwekezaji inayoitwa Central Depository System Account (Akaunti ya CDS). Akaunti hii ni tofauti na akaunti ya akiba kwa kuwa inatumika kutunza kumbukumbu na taarifa zote za uwekezaji.

Kufungua akaunti hii hakuna gharama yoyote, na mwekezaji atatakiwa kuwasilisha nyaraka za utambulisho kama vile kitambulisho cha taifa (NIDA), namba ya mlipa kodi (TIN), pamoja na picha mbili ndogo za pasipoti.

Wawekezaji wa dhamana za Serikali hupata malipo ya faida mara mbili kwa mwaka, na Benki Kuu ya Tanzania hulipa moja kwa moja stahiki hizo kupitia akaunti za benki za kila mwekezaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news