Dkt.Biteko ampa pole Rais Dkt.Mwinyi,ashiriki maziko ya kaka yake

ZANZIBAR-Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameungana na mamia ya waombolezaji kutoa pole kwa familia ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi kufuatia kifo cha kaka yake Abbas Ali Mwinyi ambaye pia alikuwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Fuoni kilichotokea Zanzibar, Unguja usiku wa kuamkia Septemba 25, 2025.
Dkt. Biteko ameshiriki maziko hayo leo Septemba 26, 2025 Bumbubwini Mangapwani, Zanzibar.

Ambapo ameungana na viongozi mbalimbali akiwemo Mgombea Mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Ndugu Stephen Wasira,Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.
Aidha, baada ya maziko baadhi viongozi walipata fursa ya kutoa heshima katika kaburi la Hayati Ali Hassan mwinyi lililopo Bumbubwini Mangapwani, Zanzibar.

Awali, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alifika msibani kuwafariji wafiwa na kisha kusaini kitabu cha maombolezo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news