DAR-Naibu Gavana wa Sera za Uchumi na Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Yamungu Kayandabila amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Tume ya Taifa ya Mipango ulioongozwa na Naibu Katibu Mtendaji anayeshughulikia Mipango ya Kitaifa, Dkt. Mursali Milanzi, tarehe 18 Septemba 2025 katika ofisi za BoT jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo yalijikita katika kujadili mikakati mbalimbali ya kugharamia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayolenga kuifanya Tanzania kuwa taifa lenye maendeleo yanayolingana na nchi zenye uchumi wa kipato cha ngazi ya juu au zaidi.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Gavana wa Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Bi. Sauda Msemo, pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Sosthenes Kewe, na viongozi wengine wa Benki Kuu.






