Dkt.Mwinyi azindua kampeni za CCM Zanzibar

ZANZIBAR-Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, tarehe 13 Septemba 2025 amezindua rasmi kampeni za Chama Cha Mapinduzi katika Uwanja wa Mnazi Mmoja, Mjini Magharibi.
Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi ameahidi kuendeleza kasi ya maendeleo kwa kuweka mkazo katika amani, elimu, afya, kilimo, ajira kwa vijana, miundombinu na uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Pia,Serikali ijayo italenga kuongeza zaidi ya ajira 350,000, kukuza uchumi (sasa ni 7.4%), kuimarisha kilimo na viwanda, kujenga maghala ya chakula, nyumba za makaazi, pamoja na kuboresha hifadhi ya jamii kwa wazee na watu wenye ulemavu.

Aidha, amesema kampeni za CCM zitakuwa za kistaarabu na kuhubiri amani, hivyo amewaomba wananchi waendelee kukiamini CCM na kumchagua yeye, Dkt.Samia Suluhu Hassan na wagombea wote wa chama hicho ili waendelee kushinda na kuijenga Zanzibar na Tanzania.
Vipaumbele vyake ni pamoja na:

✅ Elimu na Afya

✅ Kilimo na Viwanda

✅ Ujenzi wa miundombinu

✅ Ajira kwa vijana (zaidi ya 350,000)

✅ Mikopo na uwezeshaji wananchi

✅ Nyumba za makaazi na hifadhi ya jamii

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news