Magazeti leo Septemba 14,2025

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Sudan Kusini, Riek Machar, amefunguliwa mashtaka mazito ya mauaji, uhaini na uhalifu dhidi ya binadamu, hatua inayohofiwa inaweza kuibua upya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Waziri wa Sheria, Joseph Geng Akech, amesema mashitaka hayo yanahusiana na shambulio lililotokea Machi mwaka huu, linalodaiwa kufanywa na wanamgambo wanaohusishwa na Machar.
Kwa sasa barabara zinazoelekea kwenye makazi yake mjini Juba zimefungwa, huku vifaru na wanajeshi wakipewa doria.

Machar, ambaye kwa muda mrefu amekuwa mpinzani wa Rais Salva Kiir, aliwahi kuongoza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka mitano kabla ya makubaliano ya amani ya 2018.

Ingawa makubaliano hayo yalisitisha mapigano yaliyosababisha vifo vya takriban watu 400,000, mvutano kati ya Machar na Kiir umeendelea kushika kasi.

Mbali na Machar, washirika wake saba akiwemo Waziri wa Petroli, Puot Kang Chol, na Naibu Mkuu wa Majeshi, Luteni Jenerali Gabriel Duop Lam, pia wameshtakiwa na bado wako kizuizini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news