Kigida chaokoa afya ya mazingira katika uchenjuaji dhahabu

GEITA-Tume ya Madini imeendelea kutoa elimu kwa wachimbaji kuhusu matumizi ya Kigida (Retort), kifaa kinachosaidia kulinda afya za wachimbaji, mazingira na kupunguza gharama za matumizi ya zebaki katika uchenjuaji wa dhahabu.Akizungumza kwenye Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bombambili mkoani Geita, Afisa Mazingira Mwandamizi kutoka Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Geita, Hyasinta Rugeiyamu, amesema Kigida kimeundwa kwa mfumo unaozuia mvuke wa zebaki kuingia mwilini wakati wa uchenjuaji, hivyo kumlinda mchenjuaji dhidi ya madhara ya kiafya.
“Mbali na kulinda afya, Kigida huzuia pia moshi wa zebaki kutawanyika hewani. Badala yake, mvuke huo hubadilishwa kuwa kimiminika kinachohifadhiwa na kutumika tena. Hii husaidia kupunguza uchafuzi wa mazingira na gharama za ununuzi wa zebaki mpya,” amefafanua Rugeiyamu.

Ameongeza kuwa Tume ya Madini itaendelea kuhamasisha wachimbaji kote nchini kutumia Kigida ili kuhakikisha shughuli za uchenjuaji zinafanyika kwa usalama, tija na uendelevu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news