DAR-Kocha Mkuu wa Simba Sports Club (Simba SC), Fadlu Davids ametangaza kuachana na klabu hiyo kuelekea msimu ujao ambapo ameushukuru uongozi wa klabu hiyo hususani Rais Mohamed Dewji (Mo Dewji) kwa uongozi wake wa kutia moyo, maono na msaada wake wa kila mara.
Pia,Kocha huyo raia wa Afrika Kusini ambaye anahusishwa na klabu ya Raja Casablanca amewashukuru wachezaji, benchi la ufundi na mashabiki wa Simba SC kwa mshikamano na mapokezi makubwa aliyoyapata, akisisitiza kuwa klabu hiyo itaendelea kubaki sehemu ya maisha yake.
“Ni kwa moyo mzito naiaga Simba SC. Tangu nilipowasili,nilihisi shauku ya klabu hii kubwa na upendo wa mashabiki wake wa ajabu.
"Pamoja tulipambana, tukasherehekea, na tukaimarika kupitia kila ushindi na kila changamoto. Shukrani zangu za dhati kwa Rais Mo Dewji kwa uongozi wake wa kutia moyo, maono, na msaada wake wa kila mara.
“Kwa wachezaji, endeleeni kupambana, kuamini na kuilinda beji kwa heshima. Kwa mashabiki,ninyi ndio mapigo ya moyo wa klabu hii, nyimbo zenu na shauku yenu zitasikika daima katika kumbukumbu yangu. Simba itabaki sehemu yangu siku zote."
