Na Derek Kaitira MURUSURI
Kinondoni, Dar es Salaam
Sepetemba 30,2025
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan si tu kiongozi wa Tanzania; bali amejidhihirisha kuwa Kinara wa Mabadiliko na shujaa mashuhuri mwenye ushawishi mkubwa barani Afrika na duniani kote.
Akiwa Rais wa kwanza mwanamke wa Tanzania, mafanikio yake katika nyanja za siasa, uchumi, diplomasia, na maendeleo ya kijamii yanaweka rekodi za kihistoria ambazo zinathibitisha nafasi yake katika orodha ya viongozi wenye mvuto mkubwa duniani.
Uongozi wake umetajwa kuwa mfano wa jinsi nchi inaweza kurejesha utulivu wa kisiasa na kuyatumia hayo kama daraja la kufikia ukombozi wa kiuchumi.
.jpg)
.jpg)
_3.jpg)