DAR-Baada ya kuivusha Simba SC kwenda raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika,uongozi wa klabu hiyo umempa mkono wa kwaheri, kocha Hemed Suleiman (morocco) na kumshukuru kwa kuiongoza timu hiyo kwenye sare ya 1-1 dhidi ya Gaborone United na kufuzu raundi ya pili kwa ushindi wa jumla wa 2-1.
"Shukrani za dhati kwa Kocha Hemed Suleiman ‘Morocco’ kwa kuongoza kikosi chetu katika mchezo muhimu wa jana wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United, na kufanikiwa kutuvusha.
"Shukrani pia kwa Shirikisho la Soka nchini (TFF) kwa kumruhusu Kocha Morocco ambaye ni Kocha wa Taifa Stars kujiunga nasi," Simba SC.
