ZAIDI ya watu 50 wameuawa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) baada ya kushambuliwa kwa mapanga na waasi wa kundi la Allied Democratic Forces (ADF), linaloungwa mkono na kundi linalojiita Dola la Kiislamu (Islamic State), wakati wa mazishi katika kijiji cha Ntoyo, wilayani Lubero.
Afisa wa serikali katika eneo hilo, Macaire Sivikunula, alisema shambulio hilo lilitokea usiku wa kuamkia juzi.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo


























