Rais Dkt.Mwinyi aendelea kupaisha Sekta ya Michezo Zanzibar, afungua uwanja wa kisasa Kitope

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema,Serikali inalenga kufanya mageuzi makubwa ya michezo kwa kujenga na kukarabati viwanja vya kisasa ili kukuza vipaji, kuandaa wataalamu na kuiandaa Zanzibar kushiriki mashindano ya kimataifa ikiwemo AFCON 2027.
Dkt.Mwinyi ameyasema hayo leo Septemba 9,2025 alipofungua uwanja wa kisasa wa michezo uliopo Kitope, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amesema tayari ukarabati wa Amani Complex, Mao Tse Tung na Gombani umekamilika, huku viwanja vipya vikijengwa Kizimkazi (21,000), Fumba (31,000) na viwanja 17 vya mikoa na wilaya.

Halikadhalika, amesisitiza michezo kuwa nyenzo ya kuibua vipaji, ajira, utalii na kudumisha utamaduni, sambamba na ushiriki wa vijana, wanawake na makundi maalum katika mazingira rafiki na salama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news