Kivuko cha MV Bukondo kinachotarajiwa kufanya safari zake katika visiwa vya Ziwa Victoria wilayani Ukerewe mkoani Mwanza kimeshushwa kwenye maji Septemba 16, 2025 baada ya ujenzi wake kukamilika.
Ni kimoja kati ya vivuko vitano vya serikali vinavyojengwa katika karakana ya Songoro Marine wilayani Ilemela kwa gharama ya Shilingi billioni 28.
"Nipo hapa kwa niaba ya wananchi wa mkoa wa Mwanza kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi huu.
“Vivuko ni muhimu kwasababu asilimia 53 ya mkoa wa Mwanza ni maji ya ziwa Victoria. Kwahiyo shughuli za usafirishaji ni kipaumbele cha serikali yetu kuhakikisha wananchi wanaondokana na adha ya usafiri,”amesema mkuu wa Mkoa, Said Mtanda wakati wa uzinduzi wa kivuko hicho.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo














