MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Beno Malisa amewataka wenyeviti wa mitaa yote jijini Mbeya kwa kushirikiana na wananchi kulinda miundombinu ya barabarani ikiwemo taa na vyuma vya madaraja ambavyo huwekwa na serikali kwa gharama kubwa, lakini wananchi wasio waaminifu hufanya uharibufu wa makusudi na kuiba vifaa vya taa hizo.
Malisa ameeleza hayo wakati akitoa taarifa kwa wananchi juu ya ujio wa kampeni ya kupanda miti ngazi ya kaya ili kulinda mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, ambapo amesema uharibifu wa taa umekua mkubwa ndani ya jiji la Mbeya jambo ambalo haliwezi kufumbiwa macho hata kidogo na mtaa utakao shindwa kulinda taa za barabara watalazimika kuchanga kwa haraka na kurejesha miundombinu iliyoibiwa
Kuhusu kuongeza ufanisi katika kupanda miti Malisa amesema awamu hii wamepanga mikakati ambayo itawasaidia kumlazimisha kila Mkazi wa Mbeya kupanda miti kwenye mazingira yake ambapo wataanzia kwenye utoaji wa vibali vya ujenzi wa nyumba kwa kutaka kila anayejenga lazima apande miti idadi atakayo pewa na wataalamu kulingana na ukubwa wa eneo lake.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo
.jpeg)

.jpeg)



.jpeg)
















