DAR-Klabu ya Simba SC imethibitisha kumteua kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Hemed Suleiman (morocco) kuwa kocha wa muda 'Caretaker' wa klabu hiyo kwenye mechi za Kimataifa baada ya Kocha, Fadlu Davids kusitisha mkataba na Kocha Selemani Matola kuwa na kadi nyekundu.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya leo Septemba 22, 2025 na uongozi wa klabu hiyo,imeeleza kuwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemruhusu Kocha morocco kujiunga na Wekundu hao wa Msimbazi katika kipindi hiki ambacho klabu inakamilisha taratibu na mchakato wa kocha wa kudumu.
Morocco ataliongoza benchi la ufundi kuelekea mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika dhidi ya Gaborone United FC Septemba 28, 2025.

