MKUU wa Wilaya ya Ukerewe,Christopher Ngubiagai, amesisitiza kwamba ulinzi wa taifa ni jukumu la kila Mtanzania, huku akiwahimiza vijana kushiriki kikamilifu katika jeshi la akiba ili kuimarisha amani na utulivu ndani ya jamii.

Ngubiagai ametoa kauli hiyo alipokuwa akifunga mafunzo ya jeshi la akiba yaliyojumuisha kata za Namilembe, Kakukuru na Ilangara ambapo askari 72 wamehitimu mafunzo hayo yaliyohitimishwa leo katika kijiji cha Nakamwa kata ya Namilembe wilayani Ukerewe.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo



























