Magazeti leo Septemba 26,2025

TUME ya Uchaguzi ya Malawi imemtangaza, Prof. Peter Mutharika kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais kwa kupata asilimia 56 ya kura, huku mpinzani wake, Lazarus Chakwera, akipata asilimia 33.
Awali, Chakwera alikubali matokeo na kueleza azma yake ya kukabidhi madaraka kwa amani. Katika hotuba yake, Chakwera alitambua ushindi wa Mutharika na kueleza kuwa matokeo ni taswira ya nia ya pamoja ya Wamalawi kutaka mabadiliko ya serikali. Aliongeza kuwa amempigia simu Mutharika kumpongeza kwa “ushindi wake wa kihistoria.”
Chakwera alithibitisha kujaribu kuzuia matokeo mahakamani, lakini alikubali uamuzi wa tume ya uchaguzi. Aidha, aliwataka Wamalawi, pande zote, kuendelea kuishi kwa amani na kuheshimiana licha ya matokeo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news