SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewataka wazalishaji, wasambazaji, wafanyabiashara na waingizaji wa bidhaa nchini kuhakikisha bidhaa wanazozalisha au kuuza zinakidhi matakwa ya viwango na ubora ili kulinda afya za wananchi na kutimiza azma ya Serikali ya kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa bora sokoni.
Akizungumza Septemba 1, 2025 na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja Ukaguzi na Utekelezaji wa Sheria wa TBS, Bi. Nuru Mwasulama amesema kuwa, bidhaa yoyote kabla ya kutumika inapaswa kukidhi matakwa ya usalama na ubora na kupata ruhusa rasmi ya kutumika.
Aidha, Bi. Nuru amebainisha kuwa,TBS imeendelea kufanya ukaguzi sokoni ili kubaini bidhaa hafifu zisizokidhi viwango na kuondoa sokoni zile ambazo hazifai kwa matumizi ya wananchi.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo








.jpeg)












.jpeg)