CHAMA cha African Democratic Alliance (ADA-TADEA) kimesema, ili kuimarisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa mwaka 1964 watajenga daraja kutoka Bagamoyo hadi Zanzibar kurahisisha usafiri kati ya Bara na Zanzibar ili wananchi waweze kusafiri muda wowote bila vikwazo.




Ilani ya uchaguzi ya chama hicho imeeleza kuwa,daraja hilo la muungano litakuwa daraja la viwango vya hali ya juu.
Pia,imesema chama hicho kitajenga madaraja mengine Ziwa Nyasa, Victoria na Kamanga kwa ajili ya kuunganisha Wilaya ya Sengerema na Nyamagana.
Vilevile,ilani hiyo imeeleza kuwa serikali yake itayafanyia ukarabati madaraja makubwa kwenye njia kuu ya Dar es Salaam hadi Kigoma, Dar es Salaam hadi Tunduma na Mtwara hadi Mbamba Bay.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo



















