Mo Dewji amteua Crescentius Magori kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC

DAR-Rais wa Simba SC na Mwenyekiti wa Bodi, Mohammed Dewji amemteua Crescentius Magori kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Klabu ya Simba SC huku yeye akiendelea kubaki kama Mwekezaji na Rais wa Wekundu hao wa Msimbazi.
Mo Dewji ametangaza uamuzi huo Septemba 04, 2025 hatua inayokuja kutokana na majukumu yake mengine na ukweli kwamba mara nyingi yupo mbali hali iliyopelekea kuona klabu hiyo inahitaji kiongozi wa bodi ambaye yupo karibu, mwenye muda wa kutosha na anaweza kushiriki kwa ukaribu zaidi katika shughuli za kila siku.

Aidha, kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Kampuni (MEMARTS) ya Simba Sports Club Company Limited, Ibara ya 41, Mo anayo mamlaka ya kufanya uteuzi wa viongozi wa Bodi hivyo amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi upande wa Mwekezaji:

1:Barbara Gonzalez - Mjumbe wa Bodi

2:Hussein Kitta - Mjumbe wa Bodi

3:Azim Dewji - Mjumbe wa Bodi

4:Rashid Shangazi - Mjumbe wa Bodi

5:Swedi Mkwabi - Mjumbe wa Bodi

6:Zuly Chandoo Mjumbe wa Bodi

7:George Ruhango - Mjumbe wa Bodi

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news