DODOMA-Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Machibya Shiwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Bw.Abdallah Mhagama.
Mazungumzo hayo, ambayo pia yalihusisha wataalamu kutoka taasisi hizo tatu, yalifanyika katika ofisi za LATRA jijini Dodoma, na yalilenga kuboresha utendaji kazi wa TRC.


