Muhimbili-Mloganzila yaandaa kambi maalumu ya kuondoa mawe kwenye njia ya mkojo kwa teknolojia ya kisasa (Leza)

DAR-Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imeandaa kambi maalumu ya kuondoa mawe kwenye njia ya mkojo kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya Leza ambapo takribani wagonjwa 20 watanufaika na huduma hiyo ambayo itafanyika kuanzia Septemba 22 hadi 26,2025.
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Upasuaji MNH-Mloganzila, Dkt. Godlove Mfuko amesema kambi hiyo itafanywa na wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Upanga na Mloganzila kwa kushirikiana na wataalam wa MediAfric Tanzania.

Huduma hii ya kisasa hutumia kifaa maalum kinachopita kupitia njia ya mkojo kufika kwenye figo ambapo kwa msaada wa mashine ya kisasa ya leza, mawe huvunjwavunjwa na kutolewa bila kufanya upasuaji wa wazi.

Kwa mujibu wa Dkt.Mfuko watakaonufaika na huduma hii ni wale wenye changamoto za mawe kwenye figo yanayojirudia, mawe yanayoshindikana kuondolewa kwa tiba ya kawaida au yale ambayo hayafai kutibiwa kwa njia ya extracorporeal shockwave lithotripsy (ESWL).

Hivyo kwa wagonjwa wenye changamoto hiyo, wanashauriwa kufika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila kwa ajili ya kuwekwa kwenye orodha ya kuweza kupata matibabu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news