Zanzibar kujenga vituo 52 vya Afya katika bajeti ya mwaka huu

ZANZIBAR-Naibu Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya, Dkt.Fatma Mohamed Kabole amesema, Wizara ya Afya Zanzibar imepanga kujenga vituo vya afya 52 katika bajeti ya mwaka wa fedha 2025/26.
Amesema, kati ya idadi hiyo,vituo 15 vinakaribia kukamilika katika hatua ya ujenzi na vinatarajiwa kukabidhiwa kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa mwaka 2025.

Dkt.Kabole ameyasema hayo katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi huko Visitor In, Jambiani nje ya kikao kazi cha kuandaa Mpango Jumuishi wa Malezi Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto wa Miaka Mitano (5).

Kikao hicho kimefanyika mwisho mwa wiki iliyopita na kiliandandaliwa na Taasisi ya Afisi ya Rais Ufuatiliaji wa Utendaji Serikalini (PDB), Dkt.Kabole amesema,Sekta ya Afya imeimarika kwa kujenga hospitali na kuimarisha vituo vya afya katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Amesema,mbali na ujenzi wa vituo vya afya 52, Serikali imejenga hospitali 11 za wilaya ikiwemo Wilaya ya Chumbuni, Mwera Pongwe, Mbuzini, Kinyasini, kitongoje na kwingineko.

Pia amesema, zahanati 90 zinafanyiwa ukarabati na 35 zimeshakabidhiwa.

“Sekta ya Afya imeimarika sana kuanzia vifaa, dawa, hospitali zimejengwa na vituo vya afya vimeimarishwa katika Kisiwa cha Unguja na Pemba.Kila hospitali ya wilaya imewekwa vitanda 100 wakati hapo awali hospitali ya Mnazi Mmoja ilikua na vitanda 400 ni wazi kwamba Serikali ya Awamu ya Nane inayongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt.Hussein Ali Mwinyi inatekeleza ahadi zake,”amesema Dkt.Kabole.

Sambamba na hayo amesema,Hospitali ya Mkoa Lumumba imewekwa Chumba cha Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalum (ICU),hatua hiyo imekamilisha jumla ya  Vyumba vya Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalum (ICU) katika hospitali za Unguja na Pemba.

Aidha, amesema changomoto ya ukosefu wa madaktari bingwa Zanzibar,Wizara ya Afya imejipanga kuwasomesha watalaam wa ndani ili kupunguza gharama za kuajiri wataalam kutoka nje ya nchi.
Dkt.Fatma amefafanua kwamba,katika bajeti ya mwaka wa fedha 2025/26 Serikali imeiongezea wizara hiyo bajeti ya kusomesha kutoka shilingi bilioni moja hadi kufikia bilioni tatu,hatua hiyo itasaidia kuwa na wataalam wa ndani ya nchi.

Kwa upande wa wananchi akizungumza ndugu Fatma Hamad aliyejifungua katika Hospitali ya Wilaya Magogoni mwezi Agosti 15, 2025 amesema huduma inatolewa vizuri katika hospitali hiyo ila ameiomba Serikali kuongeza vitanda sehemu ya wazazi kujifungua (wodi ya wazazi) pamoja na huduma ya chakula.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news