Mkutano wa ESAAMLG wadhihirisha ufanisi wa Tanzania katika Sekta ya Fedha

ADDIS ABABA-Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania anayeshughulikia Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Bi. Sauda Kassim Msemo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Kudhibiti Fedha Haramu, ameshiriki katika Mkutano wa 25 wa Baraza la Mawaziri, Mkutano wa 50 wa Maafisa Waandamizi, pamoja na Mkutano wa 8 wa Ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Kudhibiti Fedha Haramu (ESAAMLG).
Mikutano hiyo imefanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia kuanzia tarehe 22 hadi 30 Agosti 2025, ikijadili masuala muhimu yanayohusu mapambano dhidi ya utakasishaji wa fedha haramu, pamoja na udhibiti wa ufadhili wa ugaidi na usambazaji wa silaha za maangamizi katika nchi wanachama wa ESAAMLG.
Kabla ya mikutano hiyo, kulifanyika vikao vya vikundi vya uhakiki vilivyoanzishwa kwa madhumuni ya kutathmini na kufuatilia utekelezaji wa viwango vya Kikosi Kazi cha Kimataifa cha Kudhibiti Fedha Haramu (FATF) miongoni mwa nchi wanachama.
Katika mkutano huo, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitangazwa rasmi na kupongezwa kwa kutekeleza na kukidhi viwango vya FATF, hatua inayoonesha maendeleo makubwa ya nchi katika kuimarisha mifumo ya udhibiti wa uhalifu wa kifedha na kulinda uthabiti wa sekta ya fedha.

Miongoni mwa viongozi walioshiriki mikutano hiyo ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu Mwamba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here