Rais Dkt.Mwinyi ajumuika na wananchi katika mazishi ya Sheikh Omar Bin Ali Qullaten

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amejumuika na mamia ya wananchi katika mazishi ya marehemu Sheikh Omar Bin Ali Qullaten, aliyefariki dunia jana akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Lumumba, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Alhaj Dkt. Mwinyi ameshiriki pamoja na waumini wa dini ya Kiislamu katika Sala ya kumsalia marehemu, iliyofanyika katika Msikiti wa Gofu, Mkunazini, mnamo tarehe 21 Septemba 2025.
Katika tukio hilo, Rais Mwinyi aliungana na familia, ndugu, jamaa na waumini mbalimbali kuomboleza msiba huo na kumuombea marehemu Sheikh Omar Bin Ali Qullaten apumzishwe mahali pema peponi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news