ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemteua Dkt.Mansour Maulid Mshenga kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Afya Kazini katika Ofisi ya Rais-Kazi,Uchumi na Uwekezaji Zanzibar.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena A.Said ambapo uteuzi huo umeanza leo Septemba 2,2025;
