TAKUKURU Kinondoni yafuatilia miradi ya shilingi bilioni 1

DAR-Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni, Christian Nyakizee, amesema taasisi hiyo imefuatilia miradi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja katika kipindi cha Aprili hadi Juni, 2025 na kubaini mapungufu katika baadhi ya miradi ya sekta ya afya.

Nyakizee amesema, mradi wa ujenzi wa jengo la magonjwa ya mlipuko katika Zahanati ya Kijitonyama ulionekana kuwa na gharama kubwa kuliko uhalisia, huku mradi wa jengo la upasuaji na wodi ya wazazi katika Zahanati ya Mpiji Magohe ukiwa na tatizo la madirisha kutofungwa raba vizuri, hali iliyosababisha kioo kuvunjika na maji kupenya nyakati za mvua.

Amesema, hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kuanzisha uchunguzi wa thamani ya fedha na kuwaita wadau wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ili kufanya marekebisho ya mapungufu yaliyobainika.

Aidha, amesema TAKUKURU iliendesha semina 23, mikutano ya hadhara 20, maonesho 7, vipindi vya redio 5 na kuimarisha klabu 28 za wapinga rushwa mashuleni na vyuoni, hatua iliyosaidia kuongeza usimamizi wa miradi na hamasa ya wananchi kutoa taarifa za rushwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news