Mgombea wa kiti cha Urais kupitia CCM Zanzibar, ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuwasili Pemba kesho tarehe 24 Septemba 2025, kwa ajili ya kuzungumza na Wafanyabiashara na Wajasiriamali katika Soko la Chakechake, Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
