PEMBA-Wananchi kisiwani Pemba wameonesha mapokezi makubwa kwa Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Ali Mwinyi, wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba,2025 kisiwani humo.
Maelfu ya wananchi wamejitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Gombani ya Kale, Wilaya ya Chake Chake, Mkoa wa Kusini Pemba huku wakionesha furaha na matumaini yao kwa Dkt.Mwinyi, wakisisitiza kuwa, Oktoba wanatiki kwa Dkt.Mwinyi ili kukoleza kasi ya maendeleo kote Zanzibar.#UongoziUnaoachaAlama.