DAR-Klabu ya Singida Black Stars imetwaa ubingwa wa Kombe la CECAFA Kagame 2025 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Al Hilal ya Sudan leo Septemba 15, 2025 katika dimba la KMC Complex jijini Dar es Salaam.
Clatous Chama ndiye aliyefunga mabao yote mawili ya Black Stars ambapo bao la kwanza la Chama lilifungwa dakika ya 20, lakini Al Hilal ilisawazisha dakika ya 31 kupitia Taha Abdelrazig, na timu hizo zilienda mapumziko zikiwa sare ya 1-1.Aidha,ushindi huo umewapa Singida Black Stars taji la kwanza la Kombe la Kagame, kujiunga na Simba, Yanga na Azam ambazo tayari zimeshapitia historia ya kushinda mashindano haya.
Vilevile, baada ya mchezo, Clatous Chama amepewa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mechi na Mfungaji Bora wa Mashindano, huku Metacha Mnata akishinda tuzo ya Kipa Bora.



