Serikali kuendelea kuweka ustawi bora kwa wafanyakazi wakati na baada ya utumishi

ZANZIBAR-Mkurugenzi wa Idara ya Utumishi na Uendeshaji katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar Rashid Hamdu Makame amesema Serikali itaendelea kuweka Ustawi Bora kwa Wafanyakazi wakati na baada ya Utumishi.
Mkurugenzi Idara ya Utumishi na Uendeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Rashid Hamdu Makame akifungua Mafunzo ya uwelewa kuhusu Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kwa Wafanyakazi wa Wizara hiyo huko Migombani Wilaya ya Mjini.

Ameyasema hayo wakati akifungua Mafunzo ya kuelewa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kwa wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo huko Ukumbi wa Wizara hiyo Migombani Migombani Wilaya ya Mjini.

Amesema lengo ni kuwawezesha Wafanyakazi hao, kuweza kujikimu katika kipindi cha kumalizika Utumishi wao Serikalini.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Idara ya Utumishi na Uendeshaji katika Wizara hiyo Rashid Hamdu Makame wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa wa ZSSF katika Ukumbi wa Wizara hiyo Migombani.

Amesema Serikali, inahakikisha Wafanyakazi wote wanaingiziwa Michango katika Mfuko wa ZSSF ili waweze kujipatia kipato wakati watakapomaliza muda wa Utumishi Serikalini.

Nae Afisa Uhusiano, Elimu kwa Umma kutoka Mfuko wa ZSSF Riziki Stanly amewataka Wanachama wa Mfuko huo, kufuatilia michango wanayotoa ili kuepuka kasoro zinazojitokeza wakati wanapodai mafao yao ya kustaafu.
Afisa Uhusiano Elimu kwa Umma kutoka ZSSF Riziki Stanly akitoa elimu kuhusiana na Mfuko huo, kwa Wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo huko Migombani Wilaya ya Mjini.

Aidha amesema Wanachama hao, wanatakiwa kujua kiasi cha michango walioweka, kupatiwa Vitambulisho vya Uanachama pamoja na mafao ya kiinua mgongo na Pencheni.

Kwa Upande wake Afisa Mfuko wa Hiari kutoka ZSSF Mohamed Hussein amesema Mfuko huo, unawalenga wafanyakazi wa Sekta isiokuwa rasmi kama vile Wakulima, Wavuvi, Wafugaji, Makuli, Wajasiriamali na Wanafunzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news