MWANZA-Timu tatu kutoka Klabu ya Michezo ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) zimeandika historia kwa kufuzu rasmi hatua ya 16 bora katika mashindano ya 39 ya SHIMIWI 2025 yanayofanyika jijini Mwanza kuanzia Septemba 1 hadi 16, 2025.
Hadi kufikia Septemba 5, 2025, timu tatu za TAKUKURU zimeshiriki mashindano na zote zimefuzu hatua inayofuata. Timu hizo ni ;-
📍 Kamba Wanawake
📍 Kamba Wanaume
📍 Mpira wa Miguu
Katika mashindano ya SHIMIWI 2025, pamoja na timu hizo zilizofuzu, TAKUKURU pia itashiriki kupitia timu za Riadha, Mbio za Baiskeli na Michezo ya Jadi ikiwemo Draft, ambapo timu hizo zote zinasubiri ratiba ya kuanza michezo husika.
