Aliyepokea fedha za mtego akutwa na hatia

KIGOMA-Septemba 4,2025 Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Uvinza, Mheshimiwa Misana Majura ametoa hukumu katika shauri la jinai namba 4719/2025 kati ya Jamhuri dhidi ya Bw.Jafari Hamisi Fadhili ambaye alishtakiwa kwa makosa mawili.
Ni makosa ya kuomba na kupokea rushwa kinyume na Kifungu cha 15 (1)(a) na (2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 Marejeo ya 2024.

Waendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), Bw. Amrani Buyege na Mwasiti Mshana waliiambia mahakama kuwa mshtakiwa Jafari Hamisi Fadhili mnamo Januari 4,2025 akiwa katika Kijiji cha Mgambazi ndani ya Wilaya ya Uvinza kama Afisa Mtendaji wa kujitolea, aliomba rushwa ya shilingi 3,000,000 kutoka kwa Pascal Dornald Lala ili aweze kumrudishia hati yake ya shamba.

Aidha,mahakama ilijulishwa kuwa Januari 5,2025 mshtakiwa alipokea rushwa ya shiligi 500,000 fedha ya mtego ikiwa ni sehemu ya fedha shilingi 3,000,000 alizokuwa ameomba kutoka kwa Pascal Donald Lala.

Baada ya kupitia ushahidi wa pande zote, mahakama imemtia hatiani Bw.Jafari Hamisi Fadhili na kumhukumu kulipa faini ya shilingi 500,000 kwa kila kosa au kutumikia kifungo cha miaka mitatu kwa kila kosa.Mshtakiwa alilipa faini jumla ya shilingi milioni moja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news