TCB Stawi Bond yazinduliwa rasmi,wawekezaji kupata faida asilimia 13.5 kwa mwaka

NA GODFREY NNKO

BENKI ya Biashara Tanzania (TCB) imezindua rasmi Hatifungani ya TCB Stawi Bond ambayo inampatia mwekezaji faida ya mpaka asilimia 13.5 kwa mwaka, inayolipwa kila robo mwaka.
Uzinduzi huo umefanyika leo Septemba 17,2025 jijini Dar es Salaam ukiongozwa na mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw.Elijah Mwandumbya kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dkt.Doto Biteko.

Hatua hiyo imefikiwa, baada ya Mamlaka ya Mitaji na Masoko ya Dhamana (CMSA) kuidhinisha waraka wa matarajio wa programu ya miaka mitano ya hatifungani hiyo yenye jumla ya shilingi bilioni 150.


Pia, katika toleo la kwanza CMSA imeidhinisha TCB Stawi Bond yenye jumla ya shilingi bilioni 50 huku kiwango cha chini cha kuwekeza ikiwa ni shilingi 500,000.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news