BENKI Kuu ya Tanzania imeshiriki katika Soko la jumla la Fedha za Kigeni (IFEM) kwa mujibu wa Sera yake ya ushiriki katika soko la Fedha za Kigeni ya mwaka 2023.
Katika ushiriki huu, Benki Kuu imeuza Dola za Marekani milioni 15.00 kupitia mnada wa ushindani kwa kiwango cha wastani cha kubadilisha fedha za kigeni cha Shillingi 2,471.73 kwa Dola moja ya Marekani. Lengo la mnada huu lilikuwa ni kutoa ukwasi katika soko la fedha za kigeni.

