BoT yatoa Elimu ya Fedha kwa makundi maalum Kongwa

DODOMA-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeratibu mafunzo kuhusu majukumu yake pamoja na elimu ya utambuzi wa alama za usalama katika noti za fedha na utunzaji sahihi wa noti kwa watu wenye ulemavu wilayani Kongwa mkoani Dodoma.
Mafunzo hayo yaliyofanyika leo Oktoba 21, 2025, yamehusisha makundi maalum mbalimbali wakiwemo wasioona, viziwi, walemavu wa viungo pamoja na wenye ualbino.

Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Walemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Mkoa wa Dodoma, Bw. Omary Lubuva, amesema elimu hiyo itawasaidia walemavu wanaojihusisha na ujasiriamali kuongeza ufanisi katika masuala ya kifedha.
“Kongwa ina walemavu wengi wanaojihusisha na ujasiriamali.Wengi wao hutumia na kupokea fedha, hivyo elimu hii itawawezesha kuwa makini zaidi na kushiriki ipasavyo katika shughuli za kiuchumi na ujenzi wa taifa letu,” amesema Bw.Lubuva.

Kwa upande wake, Bi.Felister Lwiwa ambaye ni mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, ameishukuru Benki Kuu kwa hatua hiyo na kuomba elimu kama hiyo kuendelea kutolewa katika maeneo mengine nchini ili walemavu wengi zaidi waweze kufaidika.
Mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi za Benki Kuu kuhakikisha wananchi wote, wakiwemo wenye ulemavu, wanapata uelewa kuhusu utunzaji sahihi wa noti na alama za usalama zinazosaidia kutambua fedha halali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news