WASHINGTON-Serikali ya Tanzania ilikutana na Timu ya Benki ya Dunia inayosimamia masuala ya benki hiyo nchini Tanzania, ikiongozwa na Mkurugenzi wake,Bw. Nathan Belete, kando ya Mkutano wa Mwaka wa 2025, kujadili maendeleo ya ushirikiano wa miradi na mipango ya maendeleo.
Ushirikiano huu unaendelea kukua, ukijumuisha miradi 30+ yenye thamani ya takriban USD 9.028 bilioni, ikilenga kuboresha maisha ya wananchi na kuhakikisha utekelezaji wa miradi kwa ufanisi.
Serikali imetambua mafanikio ya miradi ya maji na usafi wa mazingira, pamoja na Mradi wa kusaidia kaya masikini kupitia TASAF III, huku miradi mingine ya kipaumbele ikisubiri kuidhinishwa hivi karibuni.
Miradi mipya inayosubiri ridhaa ni pamoja na programu ya Agri-Connect unaolenga kuboresha kilimo, kuongeza ajira kwa vijana na wanawake, na kuimarisha usalama wa chakula.
Aidha, mpango wa National Health Compact unalenga kuimarisha mifumo ya afya kwa Uwiano wa Afya kwa wote, huku serikali ikitafuta ufadhili endelevu bila kuongeza madeni hatarishi.
Serikali pia inashirikiana na Benki katika miradi mikubwa ya miundombinu, ikiwemo Reli ya SGR na bandari, na kuendeleza sera za Policy-Based Guarantee (DPO) kusaidia kupunguza madeni ghali.
Tanzania inathibitisha dhamira yake ya kushirikiana kwa karibu na Benki ya Dunia kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa mafanikio na kuleta maendeleo kwa wananchi.





