ZANZIBAR-Mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameondoka Unguja na kuwasili Pemba.
Rais Dkt. Mwinyi anatarajiwa kukutana na wakulima wa karafuu, kukabidhi boti ya wagonjwa (ambulance), pamoja na kufunga Kampeni za Uchaguzi Mkuu za Chama Cha Mapinduzi kwa upande wa Pemba leo tarehe 23 Oktoba 2025 .





