ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametangaza Jumatano, tarehe 29 Oktoba, 2025 kuwa siku maalum ya mapumziko kwa wananchi wote wa Zanzibar.
Taarifa hiyo imetolewa leo Oktoba 23, 2025, ambapo Rais Dkt.Mwinyi amesema, uamuzi huo unalenga kuwapa wananchi wote waliokidhi vigezo nafasi ya kushiriki kikamilifu katika zoezi la kupiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amewasihi wananchi wote kufuata miongozo na maelekezo yatakayotolewa na Tume Huru ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani, utulivu na nidhamu, kama ilivyo desturi ya Zanzibar.

