Dkt.Natu Mwamba ateta na uongozi wa AfDB

WASHINGTON-Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba amemkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Bw Ronald Justin Cafrine ripoti ya utekelezaji wa shughuli za TADB kwa miaka 10 (TADB 10 years Impact Report).

Tukio hilo limefanyika katika Ubalozi wa Tanzania, kando ya Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) jijini Washington D.C nchini Marekani.
AfDB ni mdau Mkuu wa Serikali ambapo kupitia benki hiyo, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kupitia Serikali kwa nyakati tofauti, kati ya mwaka 2021 na 2024, ilipokea kiasi cha shilingi bilioni 382 kwa ajili kuimarisha mtaji ambao umechangia kwa kiasi kikubwa kuchochea ukuaji wa sekta ya kilimo na uchumi kwa wananchi.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Frank Nyabundege alieleza kuwa, AfDB imeahidi kuipatia TADB kiasi kingine cha takribani dola za Kimarekani  milioni 60 mwaka 2026 kwa ajili ya kuimarisha zaidi mtaji.
Dkt. Natu Mwamba anaongoza ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayofanyika Washington D.C, nchini Marekani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news