IMF hao,ndio wanatutambua

NA LWAGA MWAMBANDE
 
MKURUGENZI Mtendaji wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bw. Adran Ubisse ameipongeza Tanzania kwa matumizi bora ya fedha za mkopo na utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo.

Ubisse amesema,Tanzania ni mfano bora kwa nchi nyingine barani Afrika, hasa kutokana na usimamizi mzuri wa deni na sera imara za uchumi.

Pia,amesifu Mkakati wa Maendeleo wa Muda wa Kati unaotekelezwa kwa msaada wa IMF na wadau wengine.
Pongezi hizo alizitoa alipokutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba hivi karibuni katika makao makuu ya shirika hilo jijini Washington D.C nchini Marekani.

Katika mkutano huo, ulihudhuriwa pia na viongozi waandamizi kutoka Tanzania, akiwemo Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw.Emmanuel Tutuba na Balozi wa Tanzania nchini Marekani,Dkt. Elsie Kanza na wengine.

Mshairi wa kisasa, Lwaga Mwambande anabainisha kuwa,pongezi hizi za IMF kwa Tanzania ni ishara ya uaminifu wa kimataifa na zinaweza kuimarisha zaidi maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini. Endelea;

1. Imetajwa Tanzania, tena kwa uzuri sana,
Yale inajifanyia, kwamba yanafana sana,
Uchumi kusimamia, vema yatambulikana,
IMF hao, ndio wanatutambua.

2. Kwa nchi za Afrika, inafanya vema sana,
Ni nje wametamka, jinsi wanavyotuona,
Twafanya ya kutukuka, mfano mzuri sana,
IMF hao, ndio wamatutambua.

3. Mageuzi hiyo kazi, tumefanya vema sana,
Kwa bajeti na uwazi, dunia inatuona,
Mapato kupanga ngazi, ndivyo tunajulikana,
IMF hao, ndio wanatutambua.

4. Hivyo tumetambuliwa, kimataifa zaidi,
Vile tumefanikiwa, na tunavyojitahidi,
Wakubwa watuelewa, tunatimiza akidi,
IMF hao, ndio wanatutambua.

5. Kwenye mikutano yao, huko huko Marekani,
Ndiko wamesema yao, kwa tufanyavyo nchini,
Hiyo tathmini yao, inayotupa thamani,
IMF hao, ndio wanatutambua.

6. Wako viongozi wetu, uwakilishi wabeba,
Hao ni wajumbe wetu, wanafanya ya kushiba,
Ule utendaji wetu, ndio unaotubeba,
IMF hao, ndio wanatutambua.

7. Ni mengi waloyasema, hatua tusochukua,
Mifumo ya fedha myema, ni yetu tumevumbua,
Makusanyo kodi mema, yazidi kutuinua,
IMF hao, ndiyo wanatutambua.

8. Serikali za mitaa, ni zetu tunazijua,
Mifumo vyema yakaa, kwa kodi wanatanua,
Ni endelevu twajua, uchumi zatuinua,
IMF hao, ndio wanatutambua.

9. Ukuaji jumuishi, ndio tunaimarisha,
Miaka tuzidi ishi, uchumi tukingárisha,
Ndiyo wa kwetu utashi, TEHAMA tukidumisha,
IMF hao, ndio wanatutambua.

10. Lengo la uchumi wetu, mtu asiachwe nyuma,
Manufaa sote watu, yapate kuwa ni mema,
Tuendelee mbele tu, pasipo hata kukwama,
IMF hao, ndio wanatutambua.

11. Na mambo ya ubunifu, wa kifedha Tanzania,
Wajumbe wameisifu, nchi yetu Tanzania,
Ndvyo watutaarifu, ya kwamba inavutia,
IMF hao, ndio wanatutambua.

12. Ni wa kuigwa mfano, nchi yetu Tanzania,
Twaupiga mwingi mno, kiuchumi Tanzania,
Wengine watia neno, jinsi wanatusifia,
IMF hao, ndio wanatutambua.

Lwaga Mwambande (KiMPAB)
lwagha@gmauil.com 0767223602

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news