VETA yakabidhiwa vifaa vya mafunzo,vyuo 63 nchini kunufaika

DAR-Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, amekabidhi rasmi vifaa vya mafunzo vyenye thamani ya Shilingi Bilioni 8.4 kwa vyuo 63 vya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).
Makabidhiano hayo yamefanyika Oktoba 17, 2025 jijini Dar es Salaam, katika Mkutano wa VETA na Wamiliki wa Viwanda, Waajiri na Wadau wa mafunzo ya Ufundi Stadi.

Vifaa hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Serikali wa kuboresha mazingira kufundisha na kujifunza kwa vitendo.

Aidha,vifaa hivyo vimenunuliwa na Serikali kwa fedha zilizotengwa katika bajeti ya Mwaka wa fedha 2024/25 kwa lengo la kuimarisha mafunzo ya ufundi stadi nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here