GEITA-Aliyekuwa Mtia nia wa Ubunge wa Jimbo la Katoro Wilaya ya Geita, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Muambata wa Ubalozi katika kitengo cha fedha nchini Uganda, Kulwa Biteko amejitokeza kupiga kura leo Oktoba 29, 2025 katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Biteko amewahimiza wananchi wa Katoro, Busanda na Mkoa wa Geita kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kutimiza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura.





