Utulivu,amani yatawala wananchi wakiendelea kupiga kura mkoani Pwani

PWANI-Zoezi la upigaji kura mkoani Pwani linaendelea kwa amani na utulivu, ambapo Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakari Kunenge ametoa wito kwa wananchi wote wa mkoa huo kuendelea kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi hilo muhimu la kidemokrasia, akisisitiza kuwa kufanya hivyo ni haki yao ya kikatiba.
Kunenge ametoa wito huo leo Oktoba 29, 2025 mara baada ya kushiriki kupiga kura mapema asubuhi ya saa moja kwenye kituo cha Ofisi ya mkuu wa Mkoa katika uchaguzi mkuu unaofanyika kote nchini, ambapo Watanzania wanawachagua viongozi watakaoongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Akizungumza mara baada ya kupiga kura, Mh. Kunenge alisema Mkoa wa Pwani upo shwari, ulinzi umeimarishwa, hivyo kila mtu ana uhuru na usalama wa kutimiza wajibu wake wa kikatiba na akaishukuru Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa maandalizi mazuri yaliyowezesha zoezi la upigaji kura kuendelea kwa utulivu na kwa mazingira rafiki kwa wapiga kura.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news