DAR-Wanafunzi wapatao 350 kutoka Shule ya Sekondari Bagamoyo, Kisarawe II na Baobab wametembelea Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es Salaam, ambapo walipata fursa ya kujifunza kwa undani kuhusu majukumu ya Benki Kuu katika kusimamia uchumi wa nchi.

Aidha, wanafunzi hao walipata mafunzo kuhusu utambuzi wa alama za usalama katika noti za Tanzania na namna bora ya kuzitunza, ili kuepuka uharibifu wa fedha hizo.
Vilevile, wanafunzi walitembelea Makumbusho ya Benki Kuu ya Tanzania, ambako walijifunza kuhusu historia ya fedha nchini, historia ya Benki Kuu pamoja na mageuzi na maendeleo mbalimbali ya sekta ya fedha yaliyotekelezwa chini ya usimamizi wa Benki Kuu tangu kuanzishwa kwake mwaka 1966.





