NA DIRAMAKINI
MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt.Hussein Ali Mwinyi ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi tangu mwaka 2020, ameibuka kuwa miongoni mwa viongozi wa kipekee katika historia ya Zanzibar.
Ni kwa sababu ya mtazamo wake wa uongozi unaozingatia umoja wa kitaifa, mageuzi ya kiuchumi na maendeleo jumuishi ya kijamii.
Kupitia sera na mipango inayolenga ustawi wa wananchi, Dkt. Mwinyi ameweka msingi wa kuleta mageuzi ya kimfumo ambayo yameendelea kuacha alama endelevu katika historia ya Zanzibar.
Aidha, moja ya nguzo kuu ya uongozi wa Dkt. Mwinyi ni dhamira yake ya kukuza mshikamano wa kitaifa na kuimarisha maridhiano ya kisiasa kote Unguja na Pemba.
Dkt.Mwinyi amechukua hatua mahsusi za kuondoa migawanyiko ya kisiasa ambayo kwa muda mrefu iliathiri maendeleo ya Zanzibar.
Kupitia siasa za maelewano, Dkt.Mwinyi amefanikisha ushirikishwaji mpana wa wadau mbalimbali katika utendaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, hali ambayo imeongeza imani ya wananchi kwa taasisi za utawala na kuimarisha amani ya kudumu.
Pia,Dkt.Mwinyi ameanzisha na kutekeleza mikakati ya kina ya kuinua uchumi wa Zanzibar kupitia kuwekeza katika miundombinu,huduma za kijamii na sekta za kimkakati kama utalii, uvuvi na nishati.
Miongoni mwa hatua muhimu ni pamoja na ukarabati na upanuzi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja, unaolenga kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
Utekelezaji wa Sera ya Nishati ya Zanzibar 2025–2040, inayolenga kuhakikisha upatikanaji wa nishati endelevu na rafiki kwa mazingira kote Zanzibar.
Vilevile, kuna ujenzi wa miundombinu ya barabara, bandari na huduma za kijamii, ambayo imeongeza fursa za kiuchumi na kuwezesha ukuaji wa sekta binafsi.
Chini ya uongozi wa Dkt.Mwinyi, Zanzibar imeimarisha mahusiano ya kidiplomasia na nchi mbalimbali kwa lengo la kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje (FDI).
Kwa nyakati tofauti mikutano yake na viongozi wa mataifa mbalimbali duniani ikiwemo Qatar na Umoja wa Ulaya, umelenga kutangaza fursa za kiuchumi za Zanzibar na kuboresha mazingira ya biashara.
Aidha,Serikali yake imeweka mazingira rafiki kwa uwekezaji kwa kuboresha sheria na sera zinazowahusu wawekezaji.
Rais Dkt.Mwinyi ameonesha dhamira ya kuboresha maisha ya wafanyakazi wa umma kwa kuongeza mishahara, kuimarisha mazingira ya kazi na kuweka mikakati ya kuwapatia bima ya afya.
Hatua hizi ni sehemu ya juhudi za kujenga utumishi wa umma unaowajibika,unaofanya kazi kwa ufanisi,na wenye motisha ya kutoa huduma bora kwa wananchi.
Dkt.Mwinyi pia, ameweka mkazo maalum kwenye ukuzaji wa uchumi wa buluu, uchumi unaohusisha matumizi endelevu ya rasilimali za bahari kama chanzo cha mapato na ajira Zanzibar.
Hii ni pamoja na uwekezaji katika uvuvi wa kisasa, ufugaji wa samaki, uzalishaji wa mwani na utalii wa fukwe.
Kupitia sera na programu mbalimbali, serikali yake inalenga kuhakikisha kwamba rasilimali za bahari zinachangia kwa kiasi kikubwa katika pato la Taifa huku zikihifadhiwa kwa vizazi vijavyo.
Dkt.Mwinyi pia amesisitiza umuhimu wa uwazi, uwajibikaji na matumizi bora ya rasilimali za umma.
Amedhamiria na amefanikiwa kuondoa mianya ya ubadhirifu na rushwa kwa kuimarisha taasisi za udhibiti wa fedha za umma na kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Jambo hili limeongeza uwajibikaji miongoni mwa watendaji wa serikali na kuleta tija katika matumizi ya bajeti ya umma.
Ni wazi kuwa,uongozi wa Dkt.Hussein Ali Mwinyi unaendelea kuchukuliwa kama wa kipekee kwa sababu ya maono yake ya muda mrefu, utekelezaji wa sera zenye mwelekeo wa maendeleo endelevu na uwezo wake wa kusimamia mabadiliko ya kimfumo kwa amani na umoja.
Ikiwa mafanikio haya yataendelezwa na kudumishwa kwa uwajibikaji, kuna kila dalili kuwa Dkt.Mwinyi atakumbukwa kama kiongozi aliyefanikisha hatua muhimu za mageuzi ya kiuchumi, kijamii na kiutawala Zanzibar.
Hivyo,ili kumwezesha kufanya zaidi ni jukumu letu kuhakikisha Oktoba 29,2025 tunampa kura za kutosha ili miaka mitano ijayo iwe ya ushuhuda zaidi kwa mema mengi Zanzibar.
