MKUU wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Gabriel Makalla, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha miundombinu ya viwanja vya ndege vya Arusha na Manyara, hatua inayowezesha huduma za ndege kufanyika saa 24 na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa watalii.
Akizungumza Oktoba 10, 2025, wakati wa kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja, Makalla alisema maboresho hayo yameongeza ushindani na ubora wa huduma, sambamba na kuchochea ongezeko la watalii mkoani humo. “Dk. Samia amekuwa na dhamira ya kukuza utalii kupitia miundombinu rafiki inayoruhusu ndege kubwa kutua kwa saa 24,” alisema.
Aliwataka watumishi na wadau wa sekta ya usafiri wa anga kutoa huduma bora na kwa weledi ili kukuza utalii na uchumi wa mkoa. Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Arusha, Edga Mwankuga, alisema wiki ya huduma kwa mteja imetoa fursa kwa wateja kutoa maoni na kusaidia kuboresha huduma, akisisitiza kuwa “mteja ni moyo wa taasisi.”
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo

















